Skip to main content

Benki Kuu ya Dunia inataka vikwazo vya biashara ya nafaka vifutwe

Benki Kuu ya Dunia inataka vikwazo vya biashara ya nafaka vifutwe

Raisi wa Benki Kuu ya Dunia, Robert Zoellick kwenye mazungumzo aliyofanya na waandishi habari mjini Roma aliyanasihi Mataifa Wanachama kuondosha vikwazo vya biashara kwenye maeneo yao, vizuizi ambavyo anaamini ndivyo vinavyochochea kupanda kwa kasi, kwa bei za chakula katika soko la kimataifa. Alitaka vikwazo viondoshwe dhidi ya kusafirisha bidhaa za nafaka nje na pia kukomesha udhibiti wa vizuizi vyenginevyo vya kibiashara.~