Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UM Kudhibiti Akiba ya Chakula Duniani waendelea Roma

Mkutano wa UM Kudhibiti Akiba ya Chakula Duniani waendelea Roma

Mkutano Mkuu wa UM juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani unaofanyika hivi sasa mjini Roma, Utaliana leo umekamilisha siku ya pili. Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) alinakiliwa akisema “walimwengu wanalazimika, na pia kuwajibika sasa kukamilisha, kwa vitendo, haraka iwezekanavyo, yale mapendekezo ya kukabiliana na tatizo la chakula duniani,” kwa sababu, alionya, “janga la njaa limekakamaa na linaendelea kusonga mbele, kufuatilia mifumko ya bei za chakula na nishati ulimwenguni.”