Eneo zima la Darfur lizingatiwe mazingira ya uhalifu, imeonya ICC

6 Juni 2008

Luis Moreno Ocampo, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) alipohutubia kikao cha hadhara cha Baraza la Usalama Alkhamisi, kuhusu matokeo ya uchunguzi juu ya hali katika Darfur, alisema ana ushahidi wa kutosha uliothibitisha vitendo haramu vilivyokiuka kanuni za kimataifa vinafanyika kwenye eneo hilo la Sudan.

KM Ban Ki-moon, kwa kupitia msemaji wake, yeye ameinasihi Serikali ya Sudan kutekeleza majukumu yake ya kimataifa na kushirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa kulingana na sheria. Kadhalika, Risala ya KM ilisisitiza kwamba amani haitoweza kudumishwa kwenye eneo la uhasama bila ya umma kutekelezewa haki halali.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter