Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa Milenia, Mbola watathminiwa na Mtafiti Mwandamizi

Mradi wa Milenia, Mbola watathminiwa na Mtafiti Mwandamizi

Katika makala zilizopita tulijadilia juhudi za za kuondosha umasikini za wanakijiji wa Mbola, na pia kuelezea ushirikiano walionao na wataalamu wa kitaifa, na kimataifa, kwa makusudio ya kuwasilisha mafanikio ya muda mrefu kwenye eneo lao, mafanikio ambayo yatafaidisha umma, kijumla.~~

Mradi ulitaka jamii za vijijini Afrika kujinyanyua kimaisha, dhidi ya ufukara na umaskini, kwa kutumia teknolojiya ya kisasa na kutumai kadhia hiyo itasaidia kukithirisha uzalishaji wao wa kilimo, na kuimarisha huduma za afya na elimu ya msingi, na vile vile kuhakikisha ushirikishwaji wao kwenye soko za kitaifa na kimataifa utawapatia natija za kuridhisha kiuchumi.

Makala hii ni ya awali kati ya makala mbili, ambazo zitakamilisha mfululizo wa vipindi vyetu maalumu vya Redio ya UM, juu ya Mradi wa Maendeleo ya Milenia katika Mbola, Tanzania. Daktari Gershon I. Nyadzi, Mtafiti Mwandamizi wa Mradi wa Milenia katika Mbola anatathminia kwenye kipindi, taratibu zinazochukuliwa kukamilisha miradi katika ngazi za kijijini.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye mtandao.