Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jaji wa Afrika Kusini ameteuliwa kuongoza Baraza la Haki za Watumishi wa UM

Jaji wa Afrika Kusini ameteuliwa kuongoza Baraza la Haki za Watumishi wa UM

Jaji Kate O’Regan wa kutoka Afrika Kusini ameteuliwa na KM Ban Ki-moon kuwa mwenyekiti na mjumbe wa tano wa ile Tume ya Kusimamia Haki ya Ndani katika UM, bodi ambalo lilianzishwa na Baraza Kuu kwa lengo la kuhakikisha mfumo mpya wa utawala katika kazi za UM, unawakilisha chombo cha kitaalam, kilicho huru na chenye uwazi unaoaminika miongoni mwa watumishi wote wa taasisi hii ya kimataifa.~