Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Cote d'Ivoire itasaidiwa kudhibiti bora usalama wakati wa uchaguzi

Cote d'Ivoire itasaidiwa kudhibiti bora usalama wakati wa uchaguzi

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Cote d’Ivoire (UNOCI) imethibitisha ya kuwa mpango wa usalama ulioandaliwa na UM unatarajiwa kutekelezwa nchini, kuanzia wiki ijayo (Juni 19), ikiwa miongoni mwa shughuli za kutayarisha uchaguzi wa uraisi nchini. Mradi huu utahusisha mchango wa jeshi la taifa la Cote d’Ivoire, wanamgambo wa zamani wa kundi la Forces Nouvelles, vikosi vya UM viliopo Cote d\'Ivoire na katika Liberia, pamoja na majeshi ya Ufaransa ya Licorne ambayo pia yalidhaminiwa madaraka ya ulinzi nchini humo na Baraza la Usalama.