Skip to main content

Mkutano wa UNESCO unazingatia taratibu za kupunguza vurugu na siasa kali kwa vijana

Mkutano wa UNESCO unazingatia taratibu za kupunguza vurugu na siasa kali kwa vijana

Wataalamu zaidi ya 100 pamoja na vijana wa kutoka kanda zote za kimataifa, wamekusanyika Bahrain kuanzia Ijumapili tarehe 15 Juni, kwenye kikao maalumu cha kuzingatia taratibu za kuwashawishi vijana wasishiriki kwenye vitendo vya fujo inayochochewa na siasa kali, na pia kuwashawishi vijana kutoshiriki kwenye vitendo vya kutumia nguvu na mabavu.