Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP imewasilisha mradi mpya wa kuimarisha mazingira ya Nairobi

UNEP imewasilisha mradi mpya wa kuimarisha mazingira ya Nairobi

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limetangaza mradi mpya uliokusudiwa kuimarisha mazingira ya mji mkuu wa Nairobi, Kenya kwa ushirikiano na serikali, baraza la mji, wahisani wa kimataifa na vile vile Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT).

Inaaminika mradi huu utakapotekelezwa utasaidia kukuza maisha na kuongeza ajira kwa mamilioni ya raia katika Kenya.