Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BU na KM walaani miripuko ya uhasama Chad

BU na KM walaani miripuko ya uhasama Chad

KM Ban Ki-moon pamoja na Baraza la Usalama wametangaza taarifa zilizolaani, kipamoja, mfululizo wa mashambulio yalioendelezwa wiki iliopita na waasi, katika eneo la Chad mashariki. Taarifa zilionya kwamba kurejea kwa hali ya mapigano na uhasama kati ya vikosi vya Serikali na Kundi la Wapinzani la Chad ni kitendo kitakachoharibu zaidi matatizo hatari na sugu, ambayo tangu hapo awali yalikuwa yakisumbua na kudhalilisha umma katika Chad.~