Skip to main content

WFP/FAO yaashiria milioni 5 Zimbabwe watakabiliwa na njaa mwakani

WFP/FAO yaashiria milioni 5 Zimbabwe watakabiliwa na njaa mwakani

Mashirika mawili ya UM yanayohusika na chakula na kilimo, yaani mashirika ya WFP na FAO, yametoa ripoti maalumu yenye kubashiria hatari ya njaa kuzuka Zimbabwe mwanzo wa mwaka ujao, kutokana na hali mbaya ya hewa iliojiri nchini humo katika kipindi cha karibuni ambayo ilizorotisha huduma za kilimo, ikichanganyika na ukosefu wa mbolea pamoja na matatizo ya kiuchumi, kwa ujumla!