Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo na Vijana wa Afrika Mashariki juu ya Masuala ya Mazingira

Mazungumzo na Vijana wa Afrika Mashariki juu ya Masuala ya Mazingira

Kuanzia tarehe 17 mpaka 21 Juni 2008, Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP)iliandaa mkutano mkuu wa kimataifa katika mji wa Stavanger, Norway kusailia miradi ya kuhifadhi bora mazingira ulimwenguni. Mkutano ulikusanyisha wanaharakati vijana kati ya umri wa miaka 10 mpaka 14, ambao hushiriki kwenye huduma mbalimbali za kutunza mazingira katika mataifa yao. Wajumbe 700 kutoka zaidi ya mataifa 100 walihudhuria mkutano.

Tuliwahoji vijana wawili kutoka Green Garden Primary School, Kikuyu, Kenya na kijana mmoja aliyewakilisha Sungi Primary School, Moshi, Tanzania.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.