Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

GAVI inasema chanjo kinga yafaidisha afya na maendeleo kwa nchi masikini

GAVI inasema chanjo kinga yafaidisha afya na maendeleo kwa nchi masikini

Jumuiya ya Kimataifa juu ya Huduma za Chanjo Kinga dhidi ya Maradhi (GAVI) imeelezea kwenye ripoti yake ya mwaka juhudi za kimataifa za kuendeleza huduma za tiba ya chanjo kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza kwa watoto wachanga na zile huduma za kuimarisha afya ya jamii katika nchi masikini zimeonyesha mafanikio yaliopiga hatua ya kutia moyo katika kipindi cha karibuni. Jumuiya hii ya GAVI ni ya ushirikiano kati ya makampuni ya binafsi na taasisi za umma, ikijumuisha pia Shirika la Afya Duniani (WHO) na LILE lile linalohusika na maendeleo ya watoto, UNICEF.