Skip to main content

Zawadi ya UM juu ya Huduma za Jamii kutunzwa taasisi 12 za kimataifa

Zawadi ya UM juu ya Huduma za Jamii kutunzwa taasisi 12 za kimataifa

Tarehe 23 Juni huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa Siku ya Kuheshimu Mchango wa Huduma za Umma Kimataifa. Jamii ya kimataifa, kwa kuiadhimisha siku hiyo, ilizitunukia taasisi 12 za kimataifa Zawadi ya 2008 ya UM Kuhusu Huduma za Umma, taasisi ambazo kwa mchango wao kwenye huduma za kijamii zilifanikiwa kufaidisha maisha mema kwa watu wa kawaida wanaoishi kwenye maeneo yao.

Kutoka Afrika, Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watu wa Kawaida ya Rwanda pamoja na taasisi ya Afrika ya Kusini inayotoa huduma za afya kwa umma kwa kutumia reli, inayojulikana kwa Kiingereza kama Transnet-Phelophepa Health Care Train zilipewa zawadi hiyo ya UM kwa sababu ya mchango wao wa hali ya juu katika kukuza na kuimarisha maisha ya umma, kwa ujumla.