Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lampedusa kuwakumbuka wahamiaji waliopotea baharini

Lampedusa kuwakumbuka wahamiaji waliopotea baharini

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) litakuwa na taadhima maalumu Ijumamosi katika kisiwa cha Lampedusa, Utaliana ambapo kutafunguliwa rasmi mnara wa ukumbusho wa mita tano, wenye umbo la mlango unaokabili bahari inayoelekea Ulaya, uliokusudiwa kuwakumbuka maelfu ya wale wahamiaji waliopoteza maisha baharini pale walipohama makwao kutafuta maisha bora Ulaya. Mnara huo ulifinyangwa na msanii wa Kitaliana Mimmo Paladino. Mradi huu wa kumbukumbu ulijumuisha mchango wa Serikali ya Utaliana, shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR), serikali za miji ya Sicily, Puglia na Milan na pia Shirika la IOM na mashirika yasio ya kiserkali ya Kitaliana. ~