Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wa kiwango cha juu wafunguliwa Makao Makuu na ECOSOC

Mjadala wa kiwango cha juu wafunguliwa Makao Makuu na ECOSOC

Baraza la UM juu ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii (ECOSOC) Ijumatatu ya tarehe 30 Juni limeanzisha majadiliano ya kiwango cha juu, kitachoendelea mpaka Alkhamisi Julai 03 ambapo wanachama wa kimataifa watazingatia masuala yanayoambatana na taratibu za kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa duniani, hususan katika nchi zinazoendelea, pamoja kujadilia tatizo la muongezeko wa bei za chakula na nishati kwenye soko za kimataifa na vile vizingiti vinavyokwamisha na kuzorotisha juhudi za kusarifisha maendeleo.

Risala ya KM ilionya kwamba tukumbuke hakuna mfumo wo wote duniani utakaofanikiwa kuwa imara, si kiuchumi wala kijamii, pindi natija zake haziwafikii umma ulio wingi ambao hujikuta umebanwa kwenye mazingira yanayotumia utaratibu huo. Alisema tunawajibika kujiuliza kama haki ipo kwenye mfumo ambao raia matajiri 400 hukutikana kumiliki rasilmali iliokiuka mali yote wanayomiliki "umma bilioni wa tabaka la chini".