IOM inasaidia kurejesha maelfu ya Wakongamano makwao kutoka uhamishoni Zambia
Operesheni za Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) za kuwarejesha makwao maelfu ya Wakongomano waliopo Zambia, zimeanzishwa tena majuzi ambapo msafara wa watu 800 walisafirishwa kilomita 600 kutokea kambi za Kala na Mwange ziliopo majimbo ya Kaskazini na Luapula katika Zambia na kupelekwa kwenye bandari ya Mpulungu, iliopo kusini wa Ziwa Tanganyika na baadaye kupelekwa JKK.