Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wafanya ziara ya ukaguzi vijijini Kenya kuamua kurudi makwao

Wahamiaji wafanya ziara ya ukaguzi vijijini Kenya kuamua kurudi makwao

Jennifer Pagonis, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), Ijumanne aliwaambia waandishi habari Geneva kwamba wameandaa ziara maalumu ya siku moja kwa kundi la wahamiaji wa ndani ya nchi waliowakilisha wenziwao waliopo kwenye kambi za makazi ya muda, Walitembelea vijiji vyao viliopo katika eneo la Bonde la Ufa, na kuchukua fursa ya kuchunguza hali halisi ilivyo tangu walipohama mastakimu yao kwa sababu ya kuzuka mchafuko ya baada ya uchaguzi mwisho wa mwaka uliopita. Msafara wa wajumbe hawo ulitokea Nakuru. ~~

Wahamiaji wa ndani ya nchi wanatarajiwa kuzingatia kama wakati umewadia kwa wao kurejea makwao au la.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.