Skip to main content

KM achukizwa na mashambulio ya raia vijijini Darfur

KM achukizwa na mashambulio ya raia vijijini Darfur

KM Ban Ki-moon ametangaza kusikitishwa sana na mashambulio ya mabomu yaliotukia karibuni katika Darfur Kaskazini, dhidi ya raia, hususan yale mashambulio yalioharibu, kwa makusudi skuli, vituo vya maji na soko kwenye vijiji vya Um Sidir, Ein Bassar na Shegeg Karo. Vitendo hivi, alihadharisha KM, kwa kupitia msemaji wake, hukiuka sheria za kimataifa na havikubaliki kamwe. Shirika la Ulinzi wa Amani la UM katika Darfur lilisaidia kuwapeleka hospitali kwa matibabu, majeruhi wa tukio hilo vijijini.