Skip to main content

Dereva wa WFP kauawa kwenye kituo bandia cha ukaguzi Usomali

Dereva wa WFP kauawa kwenye kituo bandia cha ukaguzi Usomali

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza na kulaani vikali mauaji yaliotukia Ijumatano katika eneo la kati la Usomali, ambapo dereva aliyeajiriwa na shirika hilo alipigwa risasi na kuuawa na mwanajeshi wa mgambo wakati aliposimamishwa kwenye kituo bandia cha ukaguzi kilichopo kilomita 30 kaskazini ya Galkayo, kwenye jimbo la Mudug. WFP ilishtumu kitendo hiki ambacho ilisema ni cha pili kutukia mwaka huu na kusababisha kifo kwa watumishi wao. Ama ile shehena ya chakula ya tani za metriki 275 iliopakiwa kwenye lori husika la UM, imesalimika na haikuibiwa.~WFP iliwatumia aila ya marehemu dereva mkono wa pole na taazia.