Skip to main content

BU kuwashauri wanaohasimiana Lebanon kustahamailiana

BU kuwashauri wanaohasimiana Lebanon kustahamailiana

Alkhamisi Baraza la Usalama limetangaza taarifa iliosema "inaunga mkono" Serikali ya Lebanon, na kuyanasihi makundi yote yanayohasimiana nchini humo kujitahidi kuwacha mapigano, kuvuta subira na kuwa watulivu. Taarifa hiyo ilisomwa mbele ya waandishi habari hapa Makao Makuu na Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Mei, Balozi John Sawers wa Uingereza ambaye alisema Baraza "limeshtushwa" na kuhuzunishwa kwa "kufumka kwa mapigano Lebanon" baina ya vikundi vinavyounga mkono Serikali na kundi la upinzani la Hizb\'Allah. Balozi Sawers aliyahimiza makundi haya kuondosha vizuizi vyao walivyovitega mabarabarani ili kurudisha hali ya utulivu na amani haraka iwezekanavyo.