Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

KM Ban Ki-moon pamoja na viongozi wanaohusika na taalumu ya afya waliokusanyika Atlanta, Marekani kwenye Taasisi ya Carter wamefaikiana kuchukua hatua maalumu zitakazohakikisha uzazi salama na kukabiliana kipamoja na matatizo yanayosumbua umma dhaifu wa kimataifa unaoishi kwenye hali duni.

Djibouti imeanzisha mradi wa kukomesha ile desturi iliopitwa na wakati ya kutahiri watotowa kike. Mradi huu unasimamiwa bia na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNCEF) na vile vile Shirika la Mfuko wa Kudhibiti Idadi ya Watu Duniani (UNFPA). Kutokana na mradi huu Djibouti itakuwa ni taifa la kwanza duniani kushirikiana na taasisi za UM kukomesha tabia hatari na inayodhuru afya ya kutahiri watoto wa kike.

Kwenye makao makuu ya shirika la futboli la kimataifa la FIFA liliopo Zurich, Uswiss Ijumaa kulifikiwa makubaliano muhimu na UM ya kuongeza ushirikiano wa nguvu kati yao utakaosaidia kuimarisha kipamoja usalama na amani ya kimataifa. Mwafaka huu ulitangazwa baada ya kumalizika mazungumzo baina ya Raisi wa FIFA, Joseph S. Blatter na Wilfried Lemke, Mshauri wa KM juu ya Utumiaji wa Riadha Kukuza Amani na Maendeleo.