Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jee, sekta ya utalii Kenya ina matumaini ya kufufuka?

Jee, sekta ya utalii Kenya ina matumaini ya kufufuka?

Baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa Kenya mnamo Disemba 30, 2007 kulizuka machafuko ya kushhtusha yaliosambaa katika sehemu mbalimbali za nchi. Wiki chache tu kufuatia machafuko hayo mashirika ya kimataifa yaliripoti kwamba watu 1,500 waliuawa na raia 300,000 walilazimika kuhama mastakimu yao ili kunusurisha maisha. Watu hawa walipatiwa makazi ya muda na wenye madaraka, mbali na makwao.

Baada ya vyama vilivyogombania uchaguzi mkuu kuridhia maafikiano ya kugawana madaraka mnamo Februari 28 (2008), tunaweza kusema hali ilinyemelea kuwa tulivu Kenya, na iliwasilisha matumaini ya kutia moyo kwa shughuli za kiuchumi na jamii, kwa ujumla. Hata hivyo, sekta ya utalii bado haijafufuka kwa ukamilifu na inaendelea kuonyesha kuregarega, na inahitajia ipatiwe msukumo maalumu utakaowahamasisha watalii wa kimataifa, kwa wingi, kurejea kuitembelea Kenya, hatua ambayo ikikamilishwa itawasaidia wale raia wanaotegemea ajira kutokana na utalii kupata pato maridhawa la kuendesha maisha.

Sikiliza kwenye idhaa ya mtandao ripoti ya Mwanahabari Ann Weru, kutoka Nairobi, akisailia hali halisi katika sekta ya utalii nchini Kenya.