Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kucheleweshwa vibali vya misaada ya kiutu Myanmar kwaisumbua UM

Kucheleweshwa vibali vya misaada ya kiutu Myanmar kwaisumbua UM

KM Ban Ki-moon alikutana na waandishi habari wa kimataifa kwenye Makao Makuu ambapo aliwapatia taarifa mpya kuhusu operesheni za mashirika ya UM za kupeleka misaada ya kiutu katika Myanmar, kwa umma ulioathirika na Kimbunga Nargis kilichogharikisha sehemu kadha za nchi mnanmo tarehe 02 Mei. KM alisema mashirika ya kimataifa yamekadiria watu milioni 1.5 wamo ukingoni hatari wa kuangamia pindi misaada ya kimataifa itaendelea kucheleweshwa kuwafikia kwa sababu ya vizingiti vya kirasimu vilivyowekwa na wenye mamlaka nchini humo.

KM alitoa mwito wa dharura uitakayo Serikali ya Myanmar kuyapa umuhimu wa kiwango cha juu, kwanza kabisa, masilahi ya umma ili tujitahadhari maafa tuliyokabiliwa nayo hivi sasa yasije yakaenea na kugeuka kuwa janga lisiodhibitika tena kimataifa.