Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID, Usomali, UNMEE na mahakama za jinai ya vita kusailiwa na BU

UNAMID, Usomali, UNMEE na mahakama za jinai ya vita kusailiwa na BU

Baraza la Usalama (BU) lilitarajiwa kuzingatia ripoti ya KM kuhusu maendeleo kwenye juhudi za kueneza vikosi mseto vya UM na UA (UNAMID) katika Darfur.

Vile vile Baraza la Usalama lilitazamiwa kushauriana juu ya zile kazi za mahakama za kimataifa kuhusu Rwanda na iliokuwa Yugoslavia, na pia kuzingatia, halkadhalika, operesheni za ulinzi wa amani za UNMEE mipakani mwa Ethiopia na Eritrea, na vile vile kushauriana juu ya suala la kurudisha amani Usomali.