Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi ziada zahitajika Myanmar kuhudumia kihali waathiriwa wa Kimbunga Nargis

Juhudi ziada zahitajika Myanmar kuhudumia kihali waathiriwa wa Kimbunga Nargis

UM umeripoti kwamba siku 13 baada ya Kimbunga Nargis kugharikisha taifa la Myanmar, jumuiya ya kimataifa ilifanikiwa kupata upenu wastani, wa kuiwezesha kuhudumia umma muathiriwa misaada ya dharura ya kihali. Vile vile wahudumia misaada ya kiutu wameweza kurahisishiwa na wenye mamlaka, vibali vya kuingia Myanmar kuendeleza kazi zao.

Sikiliza taarifa zaidi kwenye idhaa ya mtandao.