Mukhtasari wa kikao cha 61 cha Baraza la Utendaji la WHO

15 Mei 2008

Kikao cha 61 cha Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO) kinatarajiwa kujumuika mjini Geneva, Uswiss kuanzia tarehe 19 mpaka 24 Mei 2008 ambapo masuala muhimu yanayohusu udhibiti bora wa matatizo ya afya ya kimataifa yatazingatiwa. Wajumbe wa kutoka Mataifa Wanachama 193 wanatazamiwa kuhudhuria kikao hiki cha mwaka.

Mwandishi habari wa Redio ya UM-Geneva, Patrick Maigua alimhoji Dktr Bill Kean, mtaalamu wa masuala ya homa ya mafua katika WHO ambaye alielezea maenedelo yalivyo kwenye mijadala ya kimataifa inayohusu mwongozo wa kukabiliana na janga la homa ya mafua, pindi likifumka.

Sikiliza fafanuzi za Dktr Kean kwenye idhaa yetu ya mtandao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter