Skip to main content

Kufifia kwa usalama Darfur kwachelewesha operesheni za UM/UA - DPKO

Kufifia kwa usalama Darfur kwachelewesha operesheni za UM/UA - DPKO

Jean-Marie Guehenno, KM Mdogo anayeongoza Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za UM (DPKO) alishtumu kwamba UM ulishindwa kutabiri mashambulizi ya mwisho wa wiki iliopita yaliofanywa na kundi la waasi wa Darfur la JEM dhidi ya Serikali ya Sudan kwa sababu ya kunyimwa misaada ya kuhudumia vyema shughuli za amani ulimwenguni.