Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu mkubwa wa chakula umetanda Ethiopia

Upungufu mkubwa wa chakula umetanda Ethiopia

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeonya ya kuwa taifa la Ethiopia linakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, kwa sababu ya kupanda kwa bei za chakula katika soko la kimataifa, na pia kutokana na kutanda kwa ukame nchini.

Matatizo yote haya yamezuka katika kipindi ambacho mashirikia ya kimataifa yenye kuhudumia misaada ya kiutu nchini Ethiopia yanakabiliwa na upungufu wa chakula na fedha zinazokadiriwa dola milioni 150 ambazo zinahitajika kukidhi mahitaji ya kazi. Mkurugenzi wa Ofisi ya OCHA, John Holmes ametoa mwito unaohimiza mchango wa kimataifa kuharakishwa kuisaidia Ethiopia kuyakabili matatizo hayo kama inavyostahiki.