Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM safarini kufuatilia huduma za dharura Myanmar

KM safarini kufuatilia huduma za dharura Myanmar

KM Ban Ki-moon amewasili Bangkok, Ijumatano na anatazamiwa kuelekea Myanmar Alkhamisi ambapo atazuru yale maeneo yaliogharikishwa na Kimbunga Nargis, na kushuhudia, binafsi, operesheni za kimataifa kuhudumia misaada ya kiutu, ya dharura, kwa waathiriwa wa tufani.

Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma mwandishi habari wa Redio ya UM, Maoqi Li, ambaye yupo safarini na KM, aliarifu kwamba mara tu baada ya kuwasili Bangkok, kwenye mkutano na waandishi habari, KM alirudia tena ile nasaha alioitoa kabla alipokuwa Makao Makuu, New York ya kwamba huu si wakati kwa jamii ya kimataifa kuchocheana mizungu ya kisiasa kuhusu msiba uliolivaa taifa la Myanmar. Alisema wajibu uliotikabili sote kwa sasa ni kuhakikisha tunafanya kila tunaloweza kuokoa maisha ya waathiriwa wa Kimbunga Nargis, kwa kuwapatia huduma za kiutu na kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, haraka iwezekanavyo.