Skip to main content

Ripoti juu ya hali ya kigeugeu ya wahamiaji wandani Kenya

Ripoti juu ya hali ya kigeugeu ya wahamiaji wandani Kenya

Hivi karibuni UM ulipokea taarifa zenye kudai wenye mamlaka nchini Kenya wameanisha shughuli za kufunga zile kambi za wahamiaji wa ndani ya nchi - au kwa lugha rasmi ya UM \'wahamiaji wa IDPs\' - ambao maelfu yao waling’olewa makwao baada ya kuzuka nchini machafuko na vurugu liliofuatilia matokeo ya uchaguzi mnamo mwisho wa 2007.

UM hatuwezi kusema kuwa watu wanalazimishwa kurudi nyumbani. Kwa sasa serekali inatueleza kuwa zaidi ya watu elfu mia moja wamerudi nyumbani, Hata hivyo, kuna wengine, kuna maelfu wengine bado wako kwenye 'camp' ya wakimbizi. Ni kweli kuwa wakimbizi wanasema wangependa tuwe na mazungumzo kati yao na wale waliowatoa nyumbani, ili wajue kuwa wakirudi huko wataweza kukaa. Hiyo wanasema; na kuna wengine pia wanasema kuwa watu wasilazimishwe kurudi, watu wawachwe waamue wenyewe kuwa ni wakati wa kurudi. Lakini hata hivyo, hatuwezi kusema kuwa watu wanalazimiswha, isipokuwa kuna maongeo nyingi kwenye redio kuomba watu kurudi, kama ni kulazimisha, labda wanaona kuwa, pengine, hawajapata wakati wa kuangalia maneno yenyewe, ili waone watarudi ama watakaa kwenye kambi ya wakimbizi; lakini vile nimesema sisi hatuwezi kusema kwa sasa kuwa watu wanalazimiswha.

Millicent pia alifahamisha majukumu ya aina gani UNHCR huyashughulikia kuhusu suala la wahamiaji wa IDPs wa Kenya:

UNHCR ni kama 'agencies' zingine; tunaweza kuzidi kusaidia watu. Tunaweza kuzidi kurudi nyumbani kuangalia vile watu wanaendelea kukaa, mipango wenye wako nayo nyumbani, tuone kama wanakaa vyema na majirani. Tunaweza pia kusaidia wakimbizi kwenda kuangalia hali ya nyumbani, ili waweze kuamua kuwa ni wakati wa kurudi. Hata hivyo, UNHCR tunafanya kazi na wengine, hatuko peke yetu, na hili jambo la kurudisha watu nyumbani ni jambo ilianzishwa na Serikali ya Kenya; na kwa sasa tunaona tunaweza kusaidia Serikali kama UNHCR. Lakini usaidizi [m]kubwa itatoka kwenye wale tunawaita 'donor community' ili wapeane zile hela [na kui]wezesha serekali kurudisha watu kwa usalama.