Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahudumia misaada ya kiutu waruhusiwa kuingia Myanmar baada KM kuonana na Kiongozi wa Taifa

Wahudumia misaada ya kiutu waruhusiwa kuingia Myanmar baada KM kuonana na Kiongozi wa Taifa

KM Ban Ki-moon Ijumaa alikutana na kiongozi wa Myanmar, Jenerali Mkuu Than Shwe kwenye mji mkuu wa Naypidaw ambako waliendeleza mazungumzo ya saa mbili yaliozingatia taratibu za kuridhisha, zitakazosaidia kipamoja kuharakisha ugawaji wa misaada ya kiutu kwa umma ulioathirika na uharibifu wa Kimbunga Nargis, ambacho kiligharikisha Myanmar, wiki tatu iliopita.