Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO imewasilisha ajenda mpya kuhusu hifadhi bora ya chakula duniani

FAO imewasilisha ajenda mpya kuhusu hifadhi bora ya chakula duniani

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limewasilisha ripoti ya ajenda muhimu yenye kuwahimiza wajumbe wa kimataifa kuizingatia kikamilifu watakapokusanyika wiki ijayo Roma, Utaliana kuhudhuria Mkutano wa Hadhi ya Juu kuhusu Hifadhi Bora ya Chakula Duniani.

Kwa mujibu wa FAO, mataifa 22, wingi wao yakiwa Afrika, hivi sasa yamebanwa na yanaonyesha udhaifu kuhusu tatizo la chakula. Mataifa yenyewe hujumuisha Eritrea, Bukini, Burundi, Comoros, Tajikistan, Sierra Leone, Liberia, Zimbabwe, Ethiopia, Haiti, Zambia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Malawi, Msumbiji, Tanzania, Guinea-Bissau, Kambodia, Korea Kaskazini, Rwanda, Botswana, Niger na Kenya.