UM waadhimisha SikuKuu ya Kimataifa Kwa Walinzi wa Amani Duniani

29 Mei 2008

Tarehe 29 Mei kila mwaka huadhimishwa na UM kuwa ni Siku Kuu ya Kimataifa Kwa Walinzi wa Amani Duniani. Leo UM umeanzisha tafrija kadha wa kadha, katika sehemu mbalimbali za dunia kuiadhimisha siku hiyo, maadhimisho ambayo yanatazamiwa kuendelea kwa mwaka mzima.

Sherehe ya mwaka huu ya Siku Kuu ya Walinzi wa Amani Duniani inaadhimisha miaka 60 tangu huduma za UM za kulinda amani zilipoanzishwa kimataifa. Hivi sasa UM umetawanya walinzi wa amani 110,000 waume kwa wake, kutoka Mataifa Wanachama 119 kwenye yale maeneo maeneo kadha ya ulimwengu yanayofufuka kutoka mazingira ya vurugu, uhasama na mapigano. Tutakupatieni ripoti maalumu kuhusu Siku Kuu ya Walinzi wa Amani baadaye katika wiki.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter