Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya Dunia itatoa dola bilioni 1.2 kupiga vita tatizo la chakula ulimwenguni

Benki ya Dunia itatoa dola bilioni 1.2 kupiga vita tatizo la chakula ulimwenguni

Benki Kuu ya Dunia imetangaza kuwa itafadhilia dola bilioni 1.2 kukabiliana kidharura na tatizo la chakula duniani, tatizo ambalo limezuka karibuni na lenye kusumbua zaidi mataifa yanayoendelea. Dola milioni 200 zinatarajiwa kutengwa zitumikie kihali zile nchi zenye uchumi dhaifu.