Skip to main content

Waburundi 300,000 wamesaidiwa kurejea mwakao na UNHCR

Waburundi 300,000 wamesaidiwa kurejea mwakao na UNHCR

Operesheni za Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) za kuwarejesha makwao, kwa khiyari, wahamiaji wa Burundi waliokuwa wakiishi kwenye kambi za muda ziliopo taifa jirani la Tanzania, kadhia zilizoanzishwa mwaka 2002, zilikamilisha kurejesha jumla ya wahamiaji 300,000 mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Zaidi ya idadi hiyo, makumi elfu ya wahamiaji wengine wa Burundi vile vile waliamua wenyewe kurejea makwao bila ya mchango wa UNHCR, hasa wale Waburundi waliokuwa wakiishi kwenye kambi ziliopo kwenye vijiji vya kaskazini-magharibi ya Tanzania. Jumla ya wahamiaji waliorejea Burundi hivi sasa ni sawa na 389,000.