Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM anafuatilia kwa ukaribu zaidi matokeo ya uchaguzi Zimbabwe

KM anafuatilia kwa ukaribu zaidi matokeo ya uchaguzi Zimbabwe

Ofisi ya Msemaji wa KM imeripoti kwamba Ban Ki-moon anafuatilia, kwa ukaribu zaidi, hali nchini Zimbabwe, hususan matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwisho wa wiki iliopita, ambapo inasemekana uorodheshaji wa hisabu ya kura unaendelea na matokeo yanatiririka polepole sana kupita kiasi.