Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM imeonya kuwa masafa marefu bado yamebakia kabla matibabu ya UKIMWI kudhibitiwa ulimwenguni

UM imeonya kuwa masafa marefu bado yamebakia kabla matibabu ya UKIMWI kudhibitiwa ulimwenguni

Ripoti ya pamoja iliotolewa na Jumuiya ya Mashirika ya UM Kupambana na UKIMWI (UNAIDS), ikijumuika na Shirika la Maendeleo ya Watoto (UNICEF) na vile vile Shirika la Afya Duniani (WHO) yamehadharisha kwamba licha ya kuwa matibabu ya UKIMWI yaliongezeka, kijumla, na kwa idadi kubwa miongoni mwa watoto waliopatwa na VVU pamoja na mama waja wazito katika sehemu kadha wa kadha za dunia, hata hivyo bado tuna masafa marefu ya kuyaendea kabla ya kushuhudia kwa mafanikio ile ahadi ya kuwa na vizazi vilivyoepukana, kihakika, na kuwa huru dhidi ya maradhi ya UKIMWI.