Hali Darfur ni ya kutisha miaka minne baada ya vurugu kuzuka
Taarifa iliotolewa mwisho wa wiki kuhusu hali katika eneo la Sudan magharibi la Darfur ilimnakili KM Ban Ki-moon akisema tangu Baraza la Usalama lilipoanza kuzingatia vurugu liliozuka eneo hilo miaka minne iliopita, hali huko ni bado ya kutisha na inaendelea kuharibika hivi sasa.