Skip to main content

WHO inaonya, hali ya hewa ya kigeugeu inahatarisha afya ya jamii

WHO inaonya, hali ya hewa ya kigeugeu inahatarisha afya ya jamii

Tarehe 07 Aprili kila mwaka hutumiwa na UM kuamsha hisia zaUM juu ya mada moja muhimu inayotakiwa kushughulikiwa kimataifa katika juhudi za kuimarisha afya bora kwa wote. Shirika la Afya Duniani (WHO) limeamua mwaka huu, 2008, kuzingatia zaidi ile mada inayohusikana na udhibiti wa dharura wa ile hatari inayokabili afya ya jamii kutokana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani. WHO ilichagua mada hii kwa kutambua ithibati ya tafiti za kimataifa kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanahatarisha usalama wa afya ya jamii katika sehemu zote za ulimwenguni.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dktr Margaret Chan kwenye risala yake ya kuadhimisha Siku ya Afya ya Kimataifa alitoa mwito ulionasihi wahisani wa kimataifa kuharakisha michango yao, ili kuzisaidia zile nchi zenye uchumi dhaifu kujiandaa kukabiliana vyema zaidi na matatizo ya afya yanayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa.