Skip to main content

Amani itarejea Kivu pakitekelezwa mwafaka wa Goma, asisitiza Mjumbe wa KM katika JKK

Amani itarejea Kivu pakitekelezwa mwafaka wa Goma, asisitiza Mjumbe wa KM katika JKK

Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM katika JKK juzi alizuru mji wa Goma na kuhudhuria mkutano wa kuimarisha amani ya eneo. Alipokuwepo huko aliyanasihi makundi yote yanayohusika na mgogoro wa jimbo hatari la Kivu, liliopo kaskazini-mashariki ya nchi, kuzitekeleza haraka ahadi walizotoa kwenye Mkutano wa Amani, Usalama na Maendeleo uliofanyika Goma mwezi Januari.