Skip to main content

UM inawakumbuka waathiriwa wa mauaji ya halaiki Rwanda

UM inawakumbuka waathiriwa wa mauaji ya halaiki Rwanda

Ijumatatu magharibi kulifanyika taadhima maalumu kwenye Makao Makuu ya UM kuwakumbuka na kuwaheshimu waathiriwa wa jinai ya mauaji yaliotukia Rwanda miaka 14 iliopita.

KM Ban Ki-moon alisema kwenye risala alioitoa katika mkusanyiko huo ya kuwa UM “unawajibika kimaadili” kuhakikisha jamii ya kimataifa inachukua kila hadhari vitendo vya mauaji ya halaiki havitoibuka tena duniani. Kwa kukamilisha pendekezo hilo ndipo KM alipolazimika kuanzisha nafasi mpya ya kuwa na Mshauri Maalumu wa Kuzuia Mauaji ya Halaiki.