Skip to main content

Mauaji ya wafuasi wa upinzani kabla uchaguzi Nepal "kushtusha" UM

Mauaji ya wafuasi wa upinzani kabla uchaguzi Nepal "kushtusha" UM

Ian Martin, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Nepal ameiambia Redio ya UM hii leo kuwa \'ameshtushwa sana\' na mauaji ya wafuasi [saba] wa Chama cha Kikomonisti Kinachofuata Itikadi za Mao Tse-Tung (Zedong) katika Wilaya ya Dung na pia mauaji ya mgombea uchaguzi mwengine mwenye kufuata siasa za KiMarx na Lenin, ambao walipigwa risasi kwenye maeneo tofauti. Imeripotiwa wafuasi wa Chama cha Kikomonisti waliuawa na vikosi vya usalama vya Nepal.