Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watumishi wawili wa UNHCR kuponea chupuchupu mashambulio ya wanamgambo Puntland

Watumishi wawili wa UNHCR kuponea chupuchupu mashambulio ya wanamgambo Puntland

Watumishi wawili wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) walisalimika chupuchupu, mwisho wa wiki iliopita, na bila ya kupata majeraha, baada ya gari lao lilipovamiwa na shambulio la kuvizia la majeshi ya mgambo, kwenye mji wa Garowe, Puntland – kaskazini-mashariki ya Usomali.

UNHCR inatumai wenye madaraka kwenye eneo la Puntland watachukua hatua za haraka kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hawo kukabili haki.