Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umma wa Mali kusini wapatiwa kinga ya homa ya manjano na chanjo ya Brazil

Umma wa Mali kusini wapatiwa kinga ya homa ya manjano na chanjo ya Brazil

Shirika la Afya Duniani (WHO) Ijumaa limeanza huduma za kuchanja watu milioni 5.7 wanaoishi Mali kusini, fadhila za mashirikiano ya awali ya mpango huu baina ya mataifa yanayoendelea kutoka shirika pekee la madawa katika Amerika ya Kusini linalotengeneza chanjo dhidi ya homa ya manjano. Kampuni ya madawa ya Brazil, inayoitwa Bio Manguinhos, ilifadhilia dozi milioni tatu za chanjo, nusu ya jumla inayohitajika kukamilisha mradi wa kupiga vita homa ya manjano katrika eneo husika. Nusu nyengine ilitolewa na kampuni ya inayotengeneza dawa ya kujikinga na homa ya manjano inayoitwa Sanofi Pasteur, shirika ambalo ujuzi wake unatambuliwa rasmi na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Uchanjaji unaofanyika Mali hivi sasa ni miongoni mwa Miradi ya Kupiga Vita Homa ya Manjano inaokadiriwa dola milioni 58 na inayofadhiliwa na GAVI, ushirikiano wa sekta za kiraia na za binafsi,wenyelengo la kupunguza hatari ya maradhi Afrika Magharibi.

Mali ni nchi ya tatu, baada ya Togo na Senegal, kuchukua hatua ya kuanzisha kampeni ya taifa ya kuwapatia raia chanjo kinga dhidi ya homa ya manjano, kampeni ambayo itafuatiwa baadaye na nchi nyengine za eneo.