FAO kuchunguza jinsi nishati ya viumbehai inavyoathiri mavuno ya chakula
Kadhalika kuanzia tarehe 14 hadi 18 Aprili Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) linaongoza mkutano maalumu kwenye mji wa Brasilia, Brazil unaohudhuriwa na mataifa ya Amerika ya Latina ambapo kati ya mada muhimu inayozingatiwa ni lile suala linalohusu udhibiti bora wa shughuli za kuzalisha nishati inayotokana na viumbehai. Lengo la majadiliano haya ni kuhakikisha mpango wa kuzalisha nishati kutokana na viumbehai hautoathiri mavuno ya chakula.