Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM kuyakaribisha maafikiano ya Serikali ya Vyama Vingi Kenya

KM kuyakaribisha maafikiano ya Serikali ya Vyama Vingi Kenya

KM wa UM Ban Ki-moon, kwa kupitia msemaji wake, ameripoti kukaribisha kwa furaha tangazo la Raisi wa Kenya, Mwai Kibaki juu ya maafikiano ya kuunda Serikali Kuu ya Vyama Vyingi, hususan vile vyama vilivyohusika moja kwa moja na mzozo uliofumka Kenya baada ya uchaguzi.

KM alivihimiza vyama vyote husika nchini Kenya kuzingatia haraka kifungu cha 4 cha ajenda ya Mazungumzo ya Upatanishi wa Taifa ili kuharakisha suluhu ya chanzo cha mvutano wao.