Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wasisitiza kilimo cha kisasa chawajibika kuzingatia mahitaji halisi ya umma masikini

Wataalamu wasisitiza kilimo cha kisasa chawajibika kuzingatia mahitaji halisi ya umma masikini

Tume ya Kimataifa Maalumu ya Wataalamu 400 waliodhaminiwa bia na Benki Kuu ya Dunia pamoja na mashirika kadha ya UM, imetoa mwito wa dharura uliojumuishwa kwenye ripoti iliopendekeza kufanyike mageuzi makali ya kimsingi, haraka iwezekanavyo, kwenye taratibu zinazotumiwa kuzalisha mazao ya chakula, ili kuhakikisha marekibisho haya mapya yatakidhi zaidi mahitaji ya watu masikini na wale wenye njaa.

Ripoti imependekeza kufungamanisha shughuli za uzalishaji chakula na malengo ya kusukuma mbele maendeleo ya jamii na hifadhi ya mazingira, ikijumuisha marekibisho katika kanuni za biashara kwenye soko la kimataifa pamoja na ule utaratibu wa serikali za mataifa yenye maendeleo ya viwandani kuwapatia posho ziada wakulima. Wataalamu hawo pia walisisitiza juu ya umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira, kwa ujumla, kwa natija za wote pote ulimwenguni.