Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO: Mitizamo ya wafanyakazi imebadilika kimawazo kwa wagonjwa wa UKIMWI

ILO: Mitizamo ya wafanyakazi imebadilika kimawazo kwa wagonjwa wa UKIMWI

Wiki hii Shirika la UM kuhusu Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO) limetoa ripoti mpya inayoelezea kupatikana marekibisho ya kutia moyo duniani, kuhusu mitizamo ya wafanyakazi wa kimataifa kwa wenziwao waliopatwa na virusi vya UKIMWI.

ILO inadhania mabadiliko haya yalipataikana kwa sababu mageuzi katika sera za kazi kuheshimu kiutu watu waliopatwa na virusi vya UKIMWI. Kadhalika makundi ya waajiri kazi na wafanyakazi huwa wanatekeleza kwa wingi Kanuni za Kuendesha Kazi za ILO kwa Waathiriwa wa Virusi vya UKIMWI.