Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali ya ndege katika JKK yaihuzunisha UM

Ajali ya ndege katika JKK yaihuzunisha UM

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limethibitisha kwamba ndege ya abiria ya kampuni ya ndege inayoitwa Hewa Bora ilianguka na kupasuka hapo Ijumanne, muda tu baada ya kuanza kuruka, katika mji wa kaskazini-mashariki wa Goma katika JKK. Iliripotiwa na Msemaji wa KM kwamba ndege ilikuwa imebeba abiria na wafanyakazi wa ndege 70 ziada.

Shirika la MONUC lilifanikiwa kutuma haraka wafanyakazi wa huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali na kuwasaidia wale watu walionusuruka na tukio hilo.