Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BU lazingatia uhusiano bora na Umoja wa Afrika

BU lazingatia uhusiano bora na Umoja wa Afrika

Baraza la Usalama (BU) asubuhi ya leo lilifanyisha kikao maalumu cha hadhi ya juu, kuzingatia taratibu mbadala, zitakazotumiwa kuimarisha uhusiano bora kati ya UM na Umoja wa Afrika, hususan katika huduma za kusawazisha usalama na amani wa kieneo na kimataifa.

Wawakilishi kutoka Mataifa Wanachama 40 ziada walitarajiwa kuzungumzia kwenye kikao hiki muhimu. Wajumbe wa Baraza la Usalama wanazingatia pia mswada wa azimio juu ya kukuza ushirikiano kati ya UM na mashirika ya kikanda, ikijumuisha Umoja wa Afrika, na azimio huenda likapigiwa kura kabla ya siku kumalizika.

Tunatumai kukupatieni ripoti zaidi kuhusu kikao cha Baraza la Usalama hapo kesho.